Mungu Baba yangu, U Mwaminifu, Hakuna geuzo ndani yako; Hubadiliki, wewe ndiwe sawa, Jana, leo na siku zijazo. Wewe Mwaminifu, Wewe Mwaminifu, Kila siku fadhili napewa; Vitu vyote ninavyo umenipa, Wewe Mwaminifu kwangu Bwana. Na viumbe vyote hulingamana, Kuonyesha utukufu wako; Jua, na mvua, mwezi tena nyota Hulishuhudia pendo lako. Samaha la dhambi, tena amani, Hivi vyote ni baraka zako; Nguvu zako zitadumu milele, Nimebarikiwa sasa kwako. Mel : William Marion Runyan 1923 [FAITHFULNESS] Text: Thomas Obediah Chisholm 1923 "Great Is Thy Faithfulness" Swahili: "Mungu ni Mwaminifu" Web : http://www.liederschatz.net